UTANGULIZI
Kabla hujaamua kufuga sungura hakikisha ya kwamba umejitoa na una muda wa
kuwahudumia wanyama hawa, ufugaji wao si rahisi kama vile ukifuga paka au mbwa,
sungura wanahitaji uangalizi na hasa kwenye usafi kwa sababu ni rahisi kwao
kupata maradhi yatokanayo na mazingira mabaya na machafu
MABANDA
Kuna aina mbili za mabanda ya kufugia kwanza ni yale ya kuwafungia ndani muda
wote bila kutoka nje na ya pili ni ile ya pili ni nusu nusu yaani wanakuwa na
mabanda na wanaweza kutoka nje kwenye ua maalumu, katika aina zote mbili ni
muhimu kuhakikisha hakuna upenyo wa kuruhusu panya kupita kwa sababu huwa
wanakula watoto wa sungura
UFUGAJI WA NDANI
1 - Usitumie
banda la kioo (aquarium) kwa sababu halina hewa ya kutosha na ni vigumu kusafisha
2 - Sakafu
ya nyavu za waya ni nzuri zaidi ila hakikisha hakuna sehemu zenye ncha kali
inayoweza kuwaumiza sungura, kwani wakiumia ni mpaka wapone wenyewe au umchinje
kwa sababu ukitumia dawa za antibiotic sungura mwili wake hauna uwezo wa kuzimeng'enya na
kuisha mwilini mwake, siku ukimchinja atabakia na dawa na hata ukinusa nyama
yake utahisi harufu ya dawa
3 - Ukubwa wa
banda usipungue mita 4 kwa 2 kwa kila sungura mmoja, likiwa kubwa zaidi ni vizuri
4 - Weka matandazio kama nyasi kavu au maranda ya mbao, lakini maranda
yatokanayo na miti yenye mafuta kama mi-pine na mikaratusi hayafai, wawekee
kipande cha blanket au taulo kwa ajili ya kulalia na kuzalia
hasa kwa wazazi
5 - Ni
muhimu kuwawekea sehemu ya kujificha mara wanapohisi hatari, unaweza kutumia
mbao, box gumu au plastiki
UFUGAJI WA NJE
1 - Sehemu
yote izungushiwe wavu wa kuku kuzuia panya kuingia na wanyama wengine kama
paka, mbwa, mwewe nk
2 - Upande
mmoja uwe na mabanda, sehemu ya chakula na maji pamoja na kivuli kwa ajili ya
sungura kupumzika
3 - Futi
moja chini ya udongo kuwe na zege kuzuia sungura kuchimba na kwenda mbali
4 - Eneo la
wazi liwe huru na hatari zote za sumu kama dawa za kuulia wadudu au mbolea, pia
majani yaliyoota yasiwe ni yale yenye sumu (waone wataalamu wakushauri au ng'oa
yote)
MAJI
Tumia
mabakuli ya kigae, plastiki au jengea kwa saruji, maji yabadilishwe kila siku
na vyombo visafishwe kila siku
CHAKULA
Wapewe
majani, mabaki ya mboga za jikoni baada ya kuchambuliwa, pia unaweza kuwawekea
pumba au chakula cha kuku (growers mash) kwenye vyombo maalumu kama chakula
chenye virutubisho (concentrates)
USAFI
Kila siku ondoa uchafu kama vyakula vilivyo mwagika, na kinyesi kilichoganda
kwenye matandazio, fagia na kubadili matandazio angalau mara moja kwa wiki,
manyoya ya sungura mzazi yasiondolewe hii huonyesha kwamba anakaribia
kuzaa watoto
MENO
Wakati
mwingine meno ya mbele hukua sana na kumsababishia usumbufu wakati wa kula,
waone wataalamu ukiona ni marefu zaidi na yanahitaji kupunguzwa, dalili kuu ni
sungura kushindwa kula kwa zaidi ya saa 12
MIGUU
Miguu ya
sungura si kama ya wanyama wengine, nyayo zake zimefunikwa kwa manyoya, angalia
ukiona yananyonyoka kuna tatizo chunguza, kucha zake nazo huhitaji kupunguzwa
zikikua sana
UBEBAJI
Usimbebe
kwa kutumia masikio yake huwa wanaumia sana, shika ngozi nyuma ya shingo kama
paka ukitaka kumbeba
Usimbebe Hivi Sungura wako
Sungura anatakiwa kubebwa hivi
DAWA
Wapewe
dawa ya minyoo kama Piperazine kila baada ya miezi mitatu, dawa za wadudu kama Akheri Powder zinyunyuziwe kwenye mabanda yao kuzuia viroboto, usiwape dawa
nyingine bila ushauri wa kitaalamu, antibiotics ndio usijaribu kabisa.
No comments:
Post a Comment