Total Pageviews

Thursday 31 December 2015

KILIMO CHA VITUNGUUMAJI

Vitunguu ni zao la mbogamboga na hulimwa kwa ajili ya balbu zake. Hulimwa nyanda za baridi kwa wingi sana.

Nyanda zenye joto vitunguu hulimwa pia. Tanzania vitunguu hulimwa sana sehemu za Mang’ula, Mgeta na Singida. Hata hivyo vitunguu hustawi maeneo mengi ya Tanzania.

Vitunguu vinaweza kulimwa mwaka mzima endapo maji yanapatikana.  Vitunguu vina matumizi mengi sana na vina madini joto,  chuma, vitamin A, vitamin B, vitamin C na vitamin E. 

HALI JOTO

Joto linatakiwa sana kwa ajili ya ukuaji wa balbu ila joto likizidi vitunguu hukomaa mapema kabla balbu hazijafikia ukubwa unaostahili, hivyo mkulima anaweza kupata mazao kidogo.

UDONGO NA MAHITAJI YA MAJI

Vitunguu huweza kupandwa kwenye udongo wowote wenye rutuba, usiotuamisha maji na usionata sana.  Hufanya vizuri kwenye udongo wenye asidi kidogo japo udongo wenye alkali kidogo sio mbaya sana. Kwenye udongo wenye mchanga mchanga umwagiliaji ni lazima. Udongo mzuri sana kwa ustawi wa vitunguu ni tifutifu-kichanga.

Umwagiliaji ni muhimu sana hasa wakati wa kuanza kutengeneza balbu. Unyevu uliozidi ni hatari sana kipindi cha ukuaji.

Epuka matumizi ya mbolea mbichi isioiva vizuri kwani husababisha vitunguu kuwa na shingo pana sana majani hukua sana badala ya balbu.

UZALISHAJI NA UPANDAJI WA VITUNGUU

Kabla ya kupanda udongo ni lazima utifuliwe vizuri na reki kuondoa mabaki ya mimea na mawe ama Vipande vikubwa vya udongo. Matuta yawe na upana wa mita moja. Vitunguu hupandwa kwa mstari mojakwamoja ama kutokea kitaluni. Pia huweza kupandwa kwa mstari pacha. Vitunguu hupandwa sm 10-15 kutoka mmea hadi mmea na sm 10-15 kutoka mstari hadi mstari.

EPUKA
Kununua mbegu za mitaani, kuzidisha sana mbolea na umwagiliaji usio na mpangilio kwani husababisha vitunguu kuzaa pacha.

Pia epuka kupanda vitunguu mahali palipopandwa mboga jamii ya vitunguu siku za nyuma. Mfano Vitunguu saumu na vitunguu majani.

KITALU CHA VITUNGUU

Ni muhimu kumwagilia maji ya kutosha siku kumi za mwanzo tangu kusia mbegu kitaluni. Vitunguu hukaa kitaluni kwa wiki 6-8 na miche ifikiapo upana wa penseli na urefu wa sm 15 ni tayari kwa kuhamishia shambani/bustanini.

AINA ZA VITUNGUU VINAVYOLIMWA TANZANIA
.  Red Creole
.  Bombay Red
.  Hybrid F1

UTUNZAJI WA SHAMBA

Kutandazia shamba na majani yaliyooza vizuri ama mabua inashauriwa ili kuongeza ruba ya ardhi, zuia magonjwa yatokanayo na udongo na magugu. Kupanda vitunguu kwenye matuta yaliyoinuka ni muhimu sana kuzuiya utuamishaji wa maji na mlipuko wa magojwa ya miche. Kungoa magugu na uvunaji ufanywe kwa mkono.

MAHITAJI YA MBOLEA

Vitunguu hufanya vizuri kama shamba litawekewa mbolea ya samadi ama mboji ilioiva vizuri. Kiasi cha tani 25-40 kwa heka kinashauriwa. Hii ni sawa na kilo 7.5 -12 kwa tuta lenye urefu wa mita 3 na upana wa mita 1.

UVUNAJI

Vitunguu huvunwa kuanzia siku 90-150 tangu kusia mbegu. Dalili za kukomaa ni kuanguka kwa majani.

Vitunguu huvunwa kwa kuvuta kwa mkono na kuhifadhiwa siku kadhaa shambani vikiwa vimefunikwa na majani. Baada ya hapo majani hukatwa na balbu hupakiwa kwa ajili ya kuhifadhi kusubiria bei nzuri. Vitunguu huweza kuhifadhiwa hadi miezi 9 tangu vivunwe bila kuharibika. Vitunguu vihifadhiwe kwenye nyuzijoto chini ya 4.4 °C ama juu ya nyuzijoto 25°C ili visiharibike.

UUZAJI

Vitunguu ni zao lenye bei nzuri ukilinganisha na mazao mengine ya mbogamboga na huuzwa kwenye masoko ya kawaida kwa bei nzuri. Kwa hivi sasa (sep. 10) hapa Morogoro vitunguu kilo moja ni Tshs. 1500/=. Kama vitunguu vikilimwa vizuri na kuhudumiwa ipasavyo Ekari moja huzaa gunia 70- 90 sawa na kg 7,000-9,000. Kama akipata soko la uhakika mkulima anaweza kupata hadi 13.5 milioni kwa msimu mmoja.








Wednesday 23 December 2015

Bilinganya Nyeupe

Zao lenye pato kubwa



Bilinganya nyeupe (Long White Eggplant) ni moja ya zao la mbogamboga ambalo lina viini lishe vingi na muhimu kama vile madini aina ya chokaa na chuma, Vitamini A, B na C, wanga, protini na maji

Kisayansi zao hili hujulikana kama Solanum Melongenai na kilimo chake huweza kufanyika katika majira yote ya mwaka.

Hali ya Hewa
Zao hili huhitaji hali ya joto la wastani, udongo wenye kina kirefu na rutuba ya kutosha na usiotuamisha maji. Kwa kawaida bilinganya hulimwa zaidi ya msimu mmoja, lakini katika nchi za kitropiki (joto) zao hili hulimwa kwa msimu mmoja.

Udongo
Zao la hili huota katika udongo wa kichanga na tifutifu, wenye rutuba ya kutosha. Unashauriwa kuweka mboji katika shamba lako ili kuurutubisha udongo vizuri.

Utayarishaji wa kitalu na usiaji
Ni muhimu kusia mbegu katika trei ili kukwepa kupotea kwa miche pamoja na kupata miche bora. Miche huchukua siku saba hadi kumi kuchipuaa, na wiki tatu hadi nne kwenye kitalu, kisha kupelekwa shambani. Ikiwa mkulima atasia mbegu ardhini, ni vyema kuandaa eneo lenye mbolea ya kutosha. Waweza kuweka mbolea ya mboji katika eneo hilo au katika matuta yako uliyoyaandaa kwa ajili ya kusia mbegu.

Upandaji wa miche
Unapopeleka miche yako shambani, hakikisha unaotesha kwa kufuata maelezo muhimu ya utaalamu ili kuweza kupata mavuno mengi na yenye ubora. Matuta ya kunyanyua yasiyotuwamisha maji hushauriwa kutumika katika kilimo cha zao hili kwani huzuia kuoza kwa mimea maji yanapotuama. Nafasi kati ya mche na mche iwe sentimeta 60 huku nafasi kati ya mstari na mstari iwe ni hatua moja. Hakikisha shamba limemwagiliwa na weka mbolea ya mboji katika kila shimo wakati wa kuotesha.

Umwagiliaji 
Zao hili likipata maji ya kutosha husitawi vizuri hivyo ni muhimu kumwagilia mara mbili hadi tatu kwa wingi kulingana na msimu husika hasa wakati wa kiangazi. Usimwagilie kipindi cha mvua kwani utasababisha bilinganya kuoza kutokana na wingi wa maji.

Palizi 
Hakikisha unafanya palizi mara kwa mara na kuacha shamba likiwa safi wakati wote ili kuondoa ushindani wa magugu na mimea kwenye chakula, maji na mwanga. Pia kuzingatia usafi kutasaidia kupunguza kuzaliana kwa wadudu waharibifu pamoja na magonjwa.

Magonjwa na wadudu
Zao hili hushambuliwa na wadudu pamoja na magonjwa ya aina mbalimbali hasa linapolimwa wakati wa kiangazi. Utitiri: Wadudu hawa kwa kiasi kikubwa wamekuwa visumbufu vya zao hili na si rahisi kukuta bilinganya haijashambuliwa na wadudu hawa, hasa wakati wa joto au kiangazi.

Kimamba: Hawa wadudu pia hushambulia bilinganya mara kwa mara wakati wa kiangazi.

Inzi weupe (white flies): Wadudu hawa kwasasa ni visumbufu vya mazao mengi ya bustani ama ya mbogamboga, na bilinganya ni moja ya mazao yanayoshambuliwa na wadudu hawa kwa kiasi kikubwa. Bilinganya inapoanza kuzaa matunda, wadudu hawa huvamia na hujikita katika majani, hufyonza maji na hatimaye bilinganya hukauka. Wadudu hawa hueneza ugonjwa unaofahamika kwa jina la Rasta. Huweza pia kusababisha majani kubadilika rangi na kuwa meusi

Barafu: Huu ndio ugonjwa mkubwa unaosumbua zao la bilinganya, na mara nyingi ugonjwa huu hutokea kipindi cha mvua. Husababisha tunda ya bilinganya kupata ukungu, kuoza na kudondoka kwenye mti. Na inaposhika tunda moja, ni rahisi kuambukiza lingine kwa haraka na matunda ya mti wote hushambuliwa. Pia wadudu kama leaf miner, bollworm, beetle pamoja na magonjwa kama root rot, leaves sports, kutu, kuoza kwa tunda, bakajani hushambulia zao hili pia.

Namna ya kudhibiti
Wadudu huweza kudhibitiwa kwa kutumia mwarobaini, tumbaku, majivu na mafuta ya taa, majani ya mustafeli pamoja na mfoori kulingana na vipimo na namna ya utengenezaji kwa maelezo sahihi kutoka kwa mtaalamu wa kilimo. Ikiwa mkulima atatumia viuatilifu, ni muhimu kutumia kulingana na ushauri wa wataalamu. Pia kuepuka kulima zao hili katika msimu ambao wadudu hao wanakuwepo kwa kasi hasa kipindi cha kiangazi.

Mavuno 
Kwa wastani, bilinganya nyeupe hutoa kilogramu 10,000 hadi 15,000 kwa ekari moja. Aina hii ya bilinganya haina tofauti sana na aina nyingine kwani huchukua siku 80 hadi 95 kukomaa na kuanza kuvunwa. Kiwango cha mavuno huongezeka mchumo baada ya mchumo, kadri siku zinavyoendelea na pia kulingana na matunzo. Bilinganya hutoa mavuno mengi na bora kwa kipindi cha miezi mitatu mfululizo, baada ya hapo mavuno huwa hafifu.


Matumizi
Mboga hii hutumika kwa ajili ya kutengeneneza saladi japo wengine pia hutumia kama mboga au kama kiungo cha chakula.






“Kanitangaze” mdudu hatari kwa nyanya









Tuta absoluta (nondo) wanataga mayai usiku kwenye sehemu ya juu ya mimea, kwenye sehemu ya chini ya majani au shina changa au sehemu za maua. Katika maisha yao, mdudu jike huweza kutaga hadi mayai 260.


Wakulima wa nyanya nchini Tanzania na maeneo jirani, wameingiwa na hofu kubwa baada ya kuenea kwa haraka mdudu hatari anaeangamiza zao la nyanya. Mdudu huyo anayejulikana kama nondo wa nyanya, na kitaalamu Tuta absoluta, aligundulika kuwepo nchini tangu mwaka 2014, lakini madhara yake yameanza kuonekana zaidi mwaka huu na anaathiri uzalishaji wa nyanya kwa kasi na kiasi kikubwa sana jambo lilopelekea wakulima kumbambika jina la “kanitangaze”. Ni muhimu kwa wakulima kumtofautisha mdudu huyu na yule mwenye mapindo, ambae kwa kawaida hushambulia nyanya na mazao mengine. Wadudu wenye mapindo ni aina ya inzi-buu lake huzalisha kijumba chembamba, ambacho husukwa kwenye majani, lakini hakishambulii tunda kama ilivyo kwa Tuta absoluta. Tuta absoluta ni nondo na buu lake huzalisha vijumba vikubwa, ambavyo hushambulia tunda la nyanya na hatimae kusababisha hasara kubwa kwa mkulima.

Tabia za wadudu hawa 
Wadudu wakubwa wanafanya kazi usiku na mapema wakati wa asubuhi. Majira ya saa 1 hadi 5 asubuhi wanaweza kuonekana wakiruka kwenye sehemu ya juu ya mmea. Muda unaobaki wa siku wanajificha kwenye sehemu ya chini ya majani. Kwa kawaida huwa wanataga mayai usiku kwenye sehemu ya juu ya mimea, kwenye sehemu ya chini ya majani au shina changa au sehemu za maua. Katika maisha yao, mdudu jike huweza kutaga hadi mayai 260. Mayai yanapoanguliwa, mabuu hutumia masaa machache kujilisha juu ya mmea. Baada ya hapo, wanaingia ndani yam mea ambapo hukaa hadi wapevuke na kuwa wadudu wakubwa. Baadhi ya mabuu walio kwenye mabadiliko huondoka kwenye pango walilopo na kuanzisha jingine, wakati mwingine ni ndani ya tunda. Buu mmoja linaweza kuharibu tunda zima kwenye shada. Wakati mabuu wanapozunguka mmea, wanafanya haraka sana kwa msaada wa nyuzi nyororo walizotengeneza.

Ukuaji 
Ukuaji wa buu hufanyika kwenye udongo na kwenye mimea yenyewe. Mdudu anapopevukia kwenye mmea, hutengeneza kijumba chenye nyuzi laini ili kujilinda. Tuta absoluta ana uwezo wa kuwa na vizazi vingi katika kipindi cha miezi 12. Katika maeneo yenye joto, mzunguko unaweza kukamilika chini ya mwezi mmoja. Kutokana na muda wa mzunguko wa maisha kuwa mfupi, kuna hatua nyingi za mdudu huyu kuharibu mmea kwa kila kipindi kimoja cha maisha yake. Wadudu hawa hawapendi baridi kali wala joto kali sana. Chini ya nyuzi joto 10 inazuia ukuaji wa mdudu huyu, na zaidi ya nyuzi joto 30 hufa.

Uharibifu 
Wadudu hawa husababisha uharibifu enezi wa jani pamoja na tunda, ambao unaweza kusababisha hasara ya asilimia 100 kwa mkulima. Mimea ya nyanya inashambuliwa kuanzia hatua za awali, hadi inapotoa matunda. Uharibifu wa awali hupelekea hatua ya pili ya maambukizi ya kuvu na bakteria. Buu linaweza kushambulia tunda mara tu linapotengenezwa. Huharibu pia vichipukizi ambavyo husababisha ukuaji mbovu wa mmea. 

Udhibiti 
Kwa kawaida utunzaji wote wa mazao hutegemea maamuzi madhubuti na utunzaji sahihi wa shamba. Kwa upande wa utunzaji wa mazao, mdudu mharibifu anatakiwa asipate chakula kwenye mmea unaomhifadhi. 

Ili kudhibiti wadudu hawa, 
zingatia mambo muhimu yafuatayo: 
• Usipande tena mazao hifadhi mara tu baada ya uzalishaji wa mazao hifadhi ya mwanzo.

• Rudia kupanda mazao yasiyokuwa jamii ya mnavu 

• Unaweza kuacha eneo hilo kwa muda wa wiki 5 hadi 6 bila kuwa na mimea hifadhi. Hali hiyo itasaidia kuondoa kizazi cha wadudu hao katika eneo hilo 

• Ondoa magugu yote yenye majani mapana. Weka mkazo kwenye kuondoa magugu jamii ya mnavu

• Ondoa mara moja masalia ya mazao ya zamani, kisha yafukie 

• Ondoa nyanya zilizoharibiwa kutoka kwenye mmea na uziteketeze 

• Kuwa makini na utendaji wa majirani katika mashamba yao 

• Pangilia eneo lako vizuri kwa kuweka nafasi kutoka katika shamba la jirani 

Shughuli za binadamu 
Mdudu huyu anasambaa kwa haraka sana kutokana na shughuli za binadamu. Ni muhimu kufanya juhudi ili kuzuia uenezaji unaotokana na shughuli hizo. 

Tuta absoluta wanaweza kutaga mayai kwenye miche iliyopo kwenye kitalu. Hivyo kabla ya kutoa miche kwenye kitalu ni lazima ichunguzwe kwa umakini, ili kuona kama kuna dalili za wadudu waharibifu. 

Endapo wafanyakazi wamekuwa kwenye shamba lililozagaa wadudu, ni muhimu kuhakikisha kuwa hawabebi wadudu kwenye nguo zao kutoka eneo moja kwenda lingine. 

Hakikisha kuwa hakuna tunda lililoathiriwa na mdudu linalopelekwa sokoni. Tunda lililoharibika liteketezwe. 

Vikapu na matenga yanayotumika kuvunia kwenye eneo lililoathirika, visipelekwe kwenye eneo safi ambalo halijaathiriwa. 

Viuatilifu 
Kuna aina nyingi za viuatilifu vinavyoweza kuua aina hii ya wadudu- “Tuta absoluta” lakini kuna mambo mengi yanayowasaidia wasife kwa urahisi. 
• “Kanitangaze” Tuta absoluta, hujificha wakati wote. Anapokuwa mkomavu hujificha chini ya majani au mabuu ndani ya majani au tunda. Hali hii hufanya viuatilifu vya mguso au kunyunyiziwa kushindwa kuleta mafanikio. 

• Mdudu huyu hujenga uwezo wa kushindana na dawa zilizotumiwa kupita kipimo. 

Ili kuweza kukabiliana na mdudu huyu, ni muhimu sana kutumia kiasi kidogo sana cha viuatilifu kwa kuwa wana uwezo wa kujenga usugu kukabiliana na dawa hizo. Au kutumia dawa za asili zinazoaminika kuwa na uwezo wa kukabiliana na aina hiyo ya wadudu. 


Tuesday 22 December 2015

PROGRAMU MPYA YA ‘PANDA MITI KIBIASHARA’ YAANZISHWA NCHINI

Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi ya Finland imeanzisha Programu ya ’Panda Miti Kibiashara’ (Private Forestry Programme).

Programu hiyo yenye makao makuu Njombe inayo madhumuni ya kuwahamasisha wananchi kupanda miti kwa kuzingatia kuwa miti ni zao la biashara.

Ingawaje Programu hiyo imeshiriki kwa mara ya kwanza katika maonyesho ya Sabasaba ilikuwa kati ya sehemu zilizowavutia watu wengi ndani banda la Maliasili na Utalii. Wananchi waliotembelea waliuliza maswali kuhususiana na aina za miti ya mbao inayofaa kupandwa katika sehemu zao na upatikanaji wake.

Programu ya Panda Miti Kibiashara inatekelezwa katika wilaya sita za Ludewa, Makete, Njombe, Kilolo, Mufindi na Kilombero. Programu hii ni ya miaka 16 lakini itatekelezwa kwa awamu za miaka minne kila moja.


Lengo la Programu hiyo  ni  kuongeza kipato cha wananchi  waishio  vijijini kwa kupanda miti. Lengo hilo litafanikiwa kama wananchi watalima mashamba ya miti kitaalamu kwa kuzingatia matumizi  ya  mbegu bora na kulihudumia shamba kitaalamu ili mazao yatakayopatikana  yaweze kuvutia soko la ndani na nje.



Lengo lingine ni kuanzisha shughuli  ya kujiongezea kipato nje ya shamba la miti wakati wahusika wakisubiri miti ifikie umri wa kuvunwa. Shughuli hizo ni kama vile kilimo cha matunda na ufugaji nyuki. Aidha wananchi  wamehimizwa kuunda vikundi vya Wakulima wa Miti ili iwe rahisi kwa Programu kutoa msaada kwao.
Kwa sasa miche ambayo itapandwa na wananchi walioko katika wilaya zinazohudumiwa na Programu inakuzwa kwenye vitalu ili iwe tayari kupandwa mwezi Desemba mwaka huu na Januari mwakani.
Programu imeazimia kuwa katika kipindi cha awamu ya kwanza ya Programu (mwaka 2014 hadi 2017) jumla ya hekta 15,000 zitapandwa na wananchi waliojiunga na Vikundi vya Wakulima wa Miti.






UFUGAJI BORA WA SUNGURA









UTANGULIZI
Kabla hujaamua kufuga sungura hakikisha ya kwamba umejitoa na una muda wa kuwahudumia wanyama hawa, ufugaji wao si rahisi kama vile ukifuga paka au mbwa, sungura wanahitaji uangalizi na hasa kwenye usafi kwa sababu ni rahisi kwao kupata maradhi yatokanayo na mazingira mabaya na machafu


MABANDA
Kuna aina mbili za mabanda ya kufugia kwanza ni yale ya kuwafungia ndani muda wote bila kutoka nje na ya pili ni ile ya pili ni nusu nusu yaani wanakuwa na mabanda na wanaweza kutoka nje kwenye ua maalumu, katika aina zote mbili ni muhimu kuhakikisha hakuna upenyo wa kuruhusu panya kupita kwa sababu huwa wanakula watoto wa sungura


UFUGAJI WA NDANI
1 - Usitumie banda la kioo (aquarium) kwa sababu halina hewa ya kutosha na ni vigumu kusafisha

2 - Sakafu ya nyavu za waya ni nzuri zaidi ila hakikisha hakuna sehemu zenye ncha kali inayoweza kuwaumiza sungura, kwani wakiumia ni mpaka wapone wenyewe au umchinje kwa sababu ukitumia dawa za antibiotic sungura mwili wake hauna uwezo wa kuzimeng'enya na kuisha mwilini mwake, siku ukimchinja atabakia na dawa na hata ukinusa nyama yake utahisi harufu ya dawa

3 - Ukubwa wa banda usipungue mita 4 kwa 2 kwa kila sungura mmoja, likiwa kubwa zaidi ni vizuri

4 - Weka  matandazio kama nyasi kavu au maranda ya mbao, lakini maranda yatokanayo na miti yenye mafuta kama mi-pine na mikaratusi hayafai, wawekee kipande cha blanket au taulo  kwa ajili ya kulalia na kuzalia hasa kwa wazazi

5 - Ni muhimu kuwawekea sehemu ya kujificha mara wanapohisi hatari, unaweza kutumia mbao, box gumu au plastiki


UFUGAJI WA NJE
1 - Sehemu yote izungushiwe wavu wa kuku kuzuia panya kuingia na wanyama wengine kama paka, mbwa, mwewe nk

2 - Upande mmoja uwe na mabanda, sehemu ya chakula na maji pamoja na kivuli kwa ajili ya sungura kupumzika

3 - Futi moja chini ya udongo kuwe na zege kuzuia sungura kuchimba na kwenda mbali

4 - Eneo la wazi liwe huru na hatari zote za sumu kama dawa za kuulia wadudu au mbolea, pia majani yaliyoota yasiwe ni yale yenye sumu (waone wataalamu wakushauri au ng'oa yote)

MAJI
Tumia mabakuli ya kigae, plastiki au jengea kwa saruji, maji yabadilishwe kila siku na vyombo visafishwe kila siku

CHAKULA
Wapewe majani, mabaki ya mboga za jikoni baada ya kuchambuliwa, pia unaweza kuwawekea pumba au chakula cha kuku (growers mash) kwenye vyombo maalumu kama chakula chenye virutubisho (concentrates)

USAFI
Kila siku ondoa uchafu kama vyakula vilivyo mwagika, na kinyesi kilichoganda kwenye matandazio, fagia na kubadili matandazio angalau mara moja kwa wiki, manyoya ya sungura mzazi yasiondolewe hii huonyesha kwamba anakaribia kuzaa watoto


MENO
Wakati mwingine meno ya mbele hukua sana na kumsababishia usumbufu wakati wa kula, waone wataalamu ukiona ni marefu zaidi na yanahitaji kupunguzwa, dalili kuu ni sungura kushindwa kula kwa zaidi ya saa 12

MIGUU
Miguu ya sungura si kama ya wanyama wengine, nyayo zake zimefunikwa kwa manyoya, angalia ukiona yananyonyoka kuna tatizo chunguza, kucha zake nazo huhitaji kupunguzwa zikikua sana

UBEBAJI
Usimbebe kwa kutumia masikio yake huwa wanaumia sana, shika ngozi nyuma ya shingo kama paka ukitaka kumbeba


Usimbebe Hivi Sungura wako







Sungura anatakiwa kubebwa hivi







DAWA
Wapewe dawa ya minyoo kama Piperazine kila baada ya miezi mitatu, dawa za wadudu kama Akheri Powder zinyunyuziwe kwenye mabanda yao kuzuia viroboto, usiwape dawa nyingine bila ushauri wa kitaalamu, antibiotics ndio usijaribu kabisa.



KUROILER

Kuroiler ni kuku wenye asili ya india na zifuatazo ni sifa zao.


1. Wanafugwa kienyeji (ni kuku wa kienyeji au una weza kuwafuga kisasa kwa kuwaweka ndani ya banda ila wawe free)




2. Hawapati magonjwa kirahisi



3. Wanaanza kutaga wakiwa na miezi 5 



4. Wanataga miaka miwili.



5. Majogoo yanafika hadi kilo 5 na mitetea 3.5kg hadi 4kg



6. Wanataga mayai 250 na zaidi kwa mwaka. 



7. Mayai yake ni fertile ila hawalalii.  Mayai hutotoleshwa kwa incubators. 


8.  Wana nyama nyingi.

  


Wasiliana nasi 0765903379, upate kuunganishwa na wauzaji;

wanauzwa kwa order Kifaranga kimoja ni shilingi 2,500/=, kuanzia vifaranga  100 na kuendelea.


Mayai ya Kuroiler


Kuroiler




Mfugaji Witness


Mfugaji Witness Rweyemamu akiwa bandani, anafuga kuku wa nyama (broiler) huko Vikawe.  Ana kuku zaidi ya 1,000.
Kwa Mawasiliano ya Manunuzi wasiliana naye kwa simu namba 0712466711

Friday 18 December 2015

MAWAZO YANAPOFANYIWA KAZI - USHUHUDA WA MAWAZO KWENDA VITENDO


Sophie Kessy - Mkulima wa Vitunguu
Ni Mwanachama na Mkulima  pia Mtangazaji wa Clouds

Asante Mungu nauona utukufu wako ...asante mwanangu kwa moyo wa kusimamia shuhuli hii sio ndogo baba am so happy and proud of you Tariq Ferreje inshalah Mungu ni mwema...we are almost there Buberwa Robert




Napenda kuchukua nafasi hii kukupongeza wewe dada Sophie Kessy kwa usikivu wako, nakumbuka siku ya kwanza ulipoomba ushauri, hadi ukakumbwa na mafuriko ambapo eneo kubwa lilisombwa na maji na kiasi kikubwa cha mazao kuchukuliwa na maji, ulinipigia na kuniomba ushauri na nilikushauri bila ya hiyana ulifanya kwa kupitia ushauri wangu na wa wadau wengine.

Wewe ni mfano wa kuigwa kwa kuwa uliamua kufuata maelekezo na sasa unaonekana shujaa.  Nafurahi sana wewe ni moja ya wapiganaji wangu.  Naomba wamama na wadada wengine mufuate  ujasiri huu naamini mtafanikiwa.

Hongera sana Sophie Kessy.




NEEMA DANDA - 0652003630









NEEMA DANDA Mwanachama na Mfugaji wa;
Kuku wa Kienyeji
Kuku wa Nyama
Kuku wa Mayai

Anapatikana Kimara - Suka


Thursday 17 December 2015

HYDROPONIC FODDER














Ni teknolojia ya kuotesha mazao kwa maji na virutubisho bila kutegemea udongo.

Ni kimea kinachooteshwa kwa kutumia mbegu za shayiri, ili kupata chakula cha mifugo, Ng'ombe, kuku, mbuzi,kondoo, nguruwe.

Ni kilimo kinachohitaji eneo dogo, maji kidogo, hakuna haja ya udongo.

FAIDA

Ni rahisi kufanya kilimo hiki mahali popote.  Husaidia kuvuna na kupata mazao mengi kwa muda wa siku 7 pia inapunguza matumizi ya fedha kwa kununua majani, pumba kwa ndege na wanyama.

Haona madhara kwa afya za wanyama na ndege.

ULIMAJI

Kilimo hiki kinahitaji;
1. Banda maalumu la ukubwa wowote.
2. Trei za plastiki au aluminiam zenye matundu (hakikisha zisiwe na material inayozalisha kutu)
3. Virutubisho kama vile Di.Grow (green)
4. Chupa za kunyunyizia maji (sprayer)
5. Mbegu za shayiri au ngano (zisiwe zimeshambuliwa na wadudu)
6. Chombo la kulowka mbegu
7. Kitambaa cheupe




Jaribio nililofanya mwenyewe 





mbuzi akila 


ng'ombe akila


kondoo akila

 Trei 



eneo dogo mavuno mengi












CHANGAMKA MKULIMA 

Kwa mawasiliano 
+255765903379
buberwamujuni@gmail.com

Facebook: FREBU Poultry Farm Page